Ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi & Uwekezaji
Mwanzo / Huduma Zetu / Ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi & Uwekezaji
Ukaguzi & Ushauri

Ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi & Uwekezaji

Ushauri makini wa ununuzi, ukaguzi wa nyaraka Wizarani, na mikakati salama ya uwekezaji wa ardhi.

Maelezo ya Kitaalamu

Kuhusu Huduma Hii

Kununua au kuwekeza kwenye ardhi kunahitaji umakini na utaalamu wa kisheria. RELAND inatoa ushauri wa kitaalamu kwa wananchi, watanzania wanaoishi nje (Diaspora), na wawekezaji ili kuepuka utapeli, kuuziwa eneo lenye mgogoro au lililotengwa kwa matumizi ya umma.

Mambo Muhimu Yanayotekelezwa (Deliverables):

Ukaguzi rasmi wa Hati Miliki (Official Search) Wizara ya Ardhi
Uhakiki wa matumizi ya ardhi (Makazi, Biashara, Viwanda, Kilimo)
Uhakiki wa hifadhi ya barabara (Road Reserve) na vyanzo vya maji
Msaada maalum kwa Watanzania wa Diaspora kununua ardhi kwa usalama
Ushauri wa kodi ya pango la ardhi (Land Rent) na tozo za halmashauri
Uhakiki wa mikataba ya mauziano na uratibu wa uhamisho wa umiliki
Hatua za Utekelezaji

Mchakato wa Kazi Hatua kwa Hatua

01

Kupokea Nyaraka za Eneo

Mteja anawasilisha nyaraka au maelezo ya eneo analotaka kununua au kuliendeleza.

02

Ukaguzi wa Kina Wizarani

Tunafanya ukaguzi rasmi katika masjala ya Wizara ya Ardhi, TARURA, na Halmashauri.

03

Ukaguzi wa Eneo Shambani

Timu yetu inatembelea eneo kukagua mipaka, hali ya udongo, barabara na majirani.

04

Ripoti ya Ushauri wa Kitaalamu

Unapokea ripoti kamili ya maandishi inayokupa mwongozo salama wa kuendelea na malipo au kusitisha.

Maswali ya Kawaida Kuhusu Ushauri wa Kitaalamu wa Ardhi & Uwekezaji

Nipo nje ya nchi (Diaspora). RELAND inanisaidiaje kununua kiwanja salama? +

Tunakufanyia ukaguzi wa kina wa kisheria, video za eneo live, kupima mipaka na kusimamia uhamisho wa hati bila kutegemea madalali au kuingizwa kwenye mikataba hewa.

Direct Consultation

Wasilisha Mahitaji Yako

Wataalamu wetu waliosajiliwa watawasiliana nawe.