Upimaji wa Ardhi (Cadastral & Topographical)
Upimaji wa kisasa wa kijiografia, uwekaji wa beacons na kuandaa ramani rasmi za upimaji (Deed Plan).
Kuhusu Huduma Hii
RELAND inatoa huduma za kitaalamu za upimaji wa ardhi (Cadastral & Topographical Surveying) jijini Arusha na kanda ya kaskazini. Kwa kutumia vifaa vya kisasa vya RTK GNSS na Total Station, wapimaji wetu waliosajiliwa wanapima mipaka kwa usahihi wa kiwango cha juu na kuandaa ramani zilizoidhinishwa na Wizara ya Ardhi.
Mambo Muhimu Yanayotekelezwa (Deliverables):
Mchakato wa Kazi Hatua kwa Hatua
Ushauri & Ukaguzi wa Kumbukumbu
Tunaanza kwa kukagua nyaraka zako na kufanya ukaguzi kwenye kumbukumbu rasmi za ramani Wizara ya Ardhi.
Upimaji wa Shamba kwa RTK GPS
Wataalamu wetu wanafika eneo la mradi na kupima mipaka yote kwa kutumia vifaa vya kiwango cha juu cha GPS na Total Station.
Uwekaji wa Beacons & Ushuhuda
Tunaweka vigingi na beacons rasmi za zege mbele ya wajumbe wa serikali ya mtaa na majirani wa eneo.
Uidhinishaji wa Ramani Wizarani
Tunaandaa na kuwasilisha ramani rasmi za upimaji (Deed Plans) kwa ajili ya kusajiliwa na Mkurugenzi wa Upimaji wa Ardhi.
Maswali ya Kawaida Kuhusu Upimaji wa Ardhi (Cadastral & Topographical)
Kwanini ninahitaji kupima ardhi kabla ya kujenga au kununua? +
Upimaji unakuhakikishia kuwa unajenga ndani ya mipaka yako halali na kukulinda dhidi ya migogoro ya kuingiliana na majirani au kununua eneo hewa.
Upimaji na uwekaji wa beacons unachukua muda gani Arusha? +
Upimaji shambani unachukua siku 1 hadi 3, na ukamilishaji wa mahesabu ya ramani unachukua wiki 1 hadi 2.
Wasilisha Mahitaji Yako
Wataalamu wetu waliosajiliwa watawasiliana nawe.